Share news tips with us here at Hivisasa

Wakulima mjini Ahero, Kaunti ya Kisumu, wanakila sababu ya kutabasamu baada ya idara ya unyunyizaji maji shamba eneo la magharibi kuanza mpango wa kupanda na kuuza mbegu za mpunga.

Afisa msimamizi wa mradi huo wa unyunyizaji maji mashamba Joel Tunoi, amesema mpango huo unalenga kuwasaidia wakulima katika maeneo kunakopadwa mchele, kutumia fedha kidogo wanaponunua mbegu za mpunga.

Aliongeza kuwa wakulima watakuwa wanatumia mbegu chache na kupata mazao mengi kinyume na hali ilivyokuwa zamani, walipokuwa wakitumia mbegu zaidi na kuishia kupata mazao kidogo.

Tunoi alisisitiza kuwa atahakikisha kuwa atashughulikia changamoto zinazowakabili wakulima wa mpunga na kusisitiza kuwa vyama vyote vya ushirika vinasimama imara ili pesa za mkulima ziwe sawa.

“Tutahakikisha tumelainisha kila taasisi katika eneo la 'Ahero Irrigation Scheme', ya kwanza kabisa ikiwa ni vyama vya ushirika,” alisema Tunoi.