Wakaazi wa mtaa wa mabanda wa Obunga wameelezea furaha yao kufuatia kuimarishwa kwa hali ya usalama katika mtaa huo hasaa nyakati za usiku.
Baadhi ya wakaazi walisema doria za kila mara ambazo zimekuwa zikitekelezwa na maafisa wa polisi katika barabara za mtaa huo na vile vile katika vichochoro vya ndani zaidi zimesaidia kuimarisha usalama eneo hilo.
Paul Ochieng mkaazi wa eneo la Segasega mtaani Obunga anashikilia kuwa hatua za kuimarisha usalama eneo hilo kutoka kwa wadau mbali mbali wakiwemo wa idara ya usalama zimefanikisha pakubwa uhuru wa kutembea na kutekeleza shuguli za usiku kama vile biashara.
"Enyewe tangu pabuniwe mradi wa kuweka taa za mwangaza kwenye barabara ‘security light’ wanabiashara wamefaidi sana kwa maana sahii tunaweza tukatembea usiku bila uoga kununua bidhaa hasaa sisi watu wa jua kali tunaofika kwa nyumba usiku wa karibu saa nne,’’ akasema Ochieng.