Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Baada ya ziara ya rais Uhuru Kenyatta kuingia wiki ya tatu, rais amezindua mradi unaoaminika kuwa mkubwa zaidi na utakawafaidi wakazi wa Kaunti zote za Pwani.

Mradi huo wa maji ambao unafahamika kama Baricho Water Project unatarajiwa kusaidia kusambaza maji safi kwenye Kaunti za Mombasa, Kilifi, Kwale na Lamu hatua ambayo inatazamwa na wakazi kuwa nafuu kubwa kwao kufuatia kukatwa kwa bidhaa ya maji mara kwa mara na shirirka la kusambaza maji maeneo hayo na kuwaacha wakazi kuhangaika.

Akizungmza katika eneo la Baricho katika Kaunti ya Kilifi wakati wa kuzindua mradi huo, rais alisema kuwa mradi huo una lengo la kuwafaidi si tu wakazi wa Kilifi bali kila Kaunti za eneo zima la Pwani na kama njia moja ya kuwapa matumaini wakazi.

Rais alisema kuwa sasa ni wakati wa kila mkazi kufurahia matunda ya maeneo yao ikizingatiwa kuwa eneo la Pwani lina maji mengi kwa sababu ya kuwa karibu na Bahari Hindi, lakini changamoto ni kupata mbiu mwafaka ya kufsafisha chumvi.

Hata hivyo, rais alisema kuwa wakazi wawe tayari kupokea miradi mingi kutoka kwa serikali na kuwataka wakazi kuonyesha moyo wa kufanya kazi na serikali yake ya Jubilee ili kufanikisha malengo ya maendeleo katika eneo la Pwani a nchi nzima.