Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mradi wa tarakilishi kwa wanafunzi katika shule za msingi za umma utafaulu baada ya rais Uhuru Kenyatta kuzindua mradi wa umeme ambao unalenga kuleta mwangaza katika mitaa, maarufu kama Street Lighting Project, siku ya Ijumaa katika jiji la Mombasa.

Rais aidha alidokeza kuwa shule zote za umma zitakuwa zimeunganishwa kabla ya mwisho wa mwezi ujao ili kufanikisha mradi huo.

Mkuu huyo wa nchi aidha aliongeza kuwa sasa serikali yake inalenga kusambaza umeme chini ya ufadhili wa serikali katika kila shule ya msingi ambapo atahakikisha kuwa ahadi zote alizotoa kwa wakenya zinatimizwa kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Akiongea katika uga wa umma wa makadara kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa mradi wa umeme, rais alisema kuwa serikali yake imeweka lengo la kuunganisha kila nyumba na kila familia kuwa na umeme kufikia mwaka wa 2020.

“Badala ya ya kuweka malengo ya kuunganishwa umeme hadi mwaka wa 2030, sasa serikali yetu imepunguza muda huo hadi 2020 na kuna kila dalili na juhudi za kuhakikisha kuwa mradi huo unafaulu ili kila mkenya afurahie kuwa namwangaza katika nyumba yake,” alisema rais.

Matamshi ya rais yaliungwa mkono na wakazi katika Kaunti ya Mombasa ambao walihudhuria hafla hiyo na kusema kuwa serikali ikiweza kufanikisha mradi huo itakuwa njia ya rahisi kufungua nafasi za kazi za kujitegemea miongoni mwa vijana ambao