Ongezeko la talaka nchini limepelekea vijana wengi kutozingatia maswala ya kuoa ama kuoana.
Haya yamesemwa na Rukia Hamisi ambaye ni mshauri wa maswala ya ndoa katika jamii eneo la Mombasa na baadhi ya sehemu katika eneo zima la Pwani.
Katika mahojiano na mwandishi habari huyu siku ya Ijumaa, katika ofisi yake jijini Mombasa, Rukia alisema kuwa vijana wengi kike kwa kiume wamekuwa na mtindo wa kuwajibika wala kuwa ari yoyote ya kutaka kuwa karibu na familia huku akisema wengi wanafanya hivyo kwa kukosa muda wa kuwaonyesha mapenzi wenzao kwenye ndoa.
Rukia ameyasema haya baada ya ripoti kutolewa na shirika la Fin acces ambalo limeonyesha kuwa Wakenya wengi siku hizi hawatilii maswala ya ndoa maanani badala yake wanazingatia masomo na kazi.
Kutokana na jamii kutoelewana na kuzungumza maswala ya jamii inapelekea vijana wengi kusahau ndoa ambapo inachangia pakubwa kupeanwa kwa talaka.
Aidha rukia amesema kuwa watu kuchanuka imechangia kwa baadhi ya vijana kuzingatia elimu pamoja na kazi kushinda vitu vingine katika maisha.
Wakati huo Rukia amesema vijana wa siku hizi wamekosa maarifa hivyo basi imepelekea wao kutotambua umuhimu wa kuona.
Rukia ametoa wito kwa wanandoa wachanga kuomba ushauri kwa watu ambao wamekuwa katika ndoa kwa mda mrefu ili wajitayarishe na changamoto za ndoa.