Mwanamume mmoja alifikishwa mahakamani mjini Mombasa Alhamisi kwa madai ya kumiliki maganda ya risasi zilizotumika kinyume cha sheria.
Noor Mohammed Janmohamed mwenye asili ya kihindi anadaiwa kupatikana na risasi bandia 507 zilizotumika zenye urefu wa milimita 5.56 katika eneo la Buxton mjini Mombasa mnamo Januari 5, 2016.
Mtuhumiwa alikana madai hayo mbele ya hakimu Diana Mochache na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja.
Kesi hiyo itasikilizwa Machi 23,2016.