Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mshukiwa wa mauaji aliyefikishwa mahakamani hiyo jana Jumatano katika mahakama ya Mombasa atasalia rumande kwa siku 14 ili kusubiri uchunguzi dhidi yake kukamilika.

Hii ni baada ya afisa wa upelelezi Martin Ojwang kuomba mahakama impe mda ziadi ili kukamilisha uchunguzi huo dhidi ya mshukiwa.

Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatano, hakimu Diana Mochache alimtaka afisa huyo kuharakisha uchunguzi huo ili mshtakiwa kufunguliwa mashtaka ya mauaji iwapo uchunguzi utabainisha alihusika kwa njia yeyote.

Mahakama ilielezwa kuwa mnamo Novemba 9, 2015 katika eneo la Namba Tano huko Likoni, mshukiwa, Mary Adhiambo anadaiwa kumdunga kisu mvulana wa umri wa miaka 22, marehemu Hamisi Juma kwa sababu ambazo hazikutajwa.

Aidha, mahakama ilielezwa kuwa marehemu alikimbizwa katika hospitali ya Likoni ambako aliaga dunia.

Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 25, 2015 ili kubaini iwapo kweli ana kesi ya kujibu.