Mahakama kuu ya Mombasa imemuachilia huru mshukiwa wa mauaji ya watu wa tatu.
Mshukiwahuyo, Majivuno Mwasambu, anadiwa kuwaua Kipchumba Kipkoech, Abdul Azizi na Alex Ngugi kwa kuwarushia kilipuzi walipokuwa ndani ya gari aina ya Lori mnamo Agosti 29, 2012 katika eneo la Mwandoni huko Kisauni.
Akitoa uamzi huo siku ya Alhamisi, jaji katika Mahakama kuu ya Mombasa Martin Muya alisema kuwa upande wa mashtaka ulikosa kuwasilisha ushahidi wa kutosha wa kumuhusisha mshukiwa huyo na mauaji hayo.
Aidha, alisema kuwa mashahidi wote wa kesi hiyo walishindwa kuelezea iwapo walimuona mshukiwa akirusha kilipuzi hicho.
Mshukiwa huyo alijawa na fura baada ya kusikia ameachiliwa huru na Mahakama kuu ya Mombasa.