Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Jamaa anayedaiwa kumuuwa mpwa wake amefikishwa mbele ya mahakama ya Nakuru Jumatatu kujibu mashtaka.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa kwa jina Samwel Maina alimuuwa mpwa wake mnamo mwezi Disemba katika mtaa wa Kiamunyeki mjini Nakuru.

Mshtakiwa huyo hakutakiwa kujibu shtaka hilo.

Mahakama kupitia kwa jaji Maureen Odero imeagiza mshtakiwa huyo afikishwe kwenye hospitali kufanyiwa uchunguzi wa kiakili.

Kesi hiyo sasa itatajwa mwezi Februari tarehe 8 mwaka huu.