Share news tips with us here at Hivisasa

Mshukiwa wa ugadi anayehusishwa na ulipuzi wa hoteli ya Bella Vista ameshikilia msimamo wake wa awali wa kukanusha kuhusika katika ulipuzi huo wa mwaka 2012.

Thabiti Jamaldin Yahya alisisitiza kuwa hakuhusika na ulipuzi huo, bali alijipata hospitalini akiwa hali mbaya na kuongeza kuwa alikuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi huku akihusishwa na ulipuzion huo.

Aidha, aliongeza kuwa yeye pia ni mmoja kati ya majeruhi walioathirika na ulipuzi huo wala si gaidi, huku akikanusha madai kuwa alikuwa na njama ya kukata tikiti ya kuelekea Nairobi siku mmoja tu baada ya tukio hilo.

Thabit aliongeza kuwa yeye alikuwa mfanyibiashara wa nguo kwa muda wa miezi minne jijini Mombasa kabla ya kuhusishwa na ulipuzi huo.

Thabit aliyasema haya siku ya Alhamisi alipokuwa akitoa ushahidi wake katika mahakama kuu ya Mombasa.

Mnamo Mei 15, 2015, Thabit anadaiwa kuhusika katika ulipuzi wa hoteli ya Bella Vista na kusababisha mauwaji ya Mary Cheptirim na wengine kadha kupata majeraha.

Kesi yake itasikizwa tena Januari 29,2016.