Share news tips with us here at Hivisasa

Mshukiwa mmoja wa ugaidi alitiwa mbaroni siku ya Jumatatu jioni mjini Mombasa. 

Mshukiwa huyo kutoka Malindi alijisalimisha kwa polisi akiandamana na babake na kuhojiwa na maafisa wa polisi wa kitengo cha kupambana na ugaidi ATPU na maafisa wa CID.

Duru za kuaminika zinaarifu kuwa mshukiwa huyo alijisalimisha kwa polisi baada ya picha yake kutolewa kwa umma kama mmoja wa washukiwa wanaotafutwa.

Haya yanajiri baada ya polisi kumkamata mshukiwa mmoja kwa madai sawia na hayo, na kunasa silaha hatari zikiwemo bunduki, risasi na gurunedi ndani ya nyumba moja eneo la majengo.

Siku ya Jumatatu maafisa wa polisi walitoa majina na picha za washukiwa wa ugaidi ambao wanatafutwa katika eneo la Pwani, kama njia mojawapo ya kupambana na visa vya uhalifu na ugaidi.