Mshukiwa mmoja wa ugadi atasalalia korokoroni kwa siku 30 huku akisubiri uchunguzi dhidi yake kukamilika.
Hii ni baada ya maafisa wa kupambana na ugaidi kuwasilisha ombi hilo siku ya Jumanne katika mahakama ya Mombasa kutaka mshukukiwa wa ugaidi Abdifatah Twahir Abdalla, aliyekamatwa siku ya Jumatatu kwa madai ya ugadi.
Kiongozi wa mashtaka Eugine Wangila aliiambia mahakama kuwa mshukiwa huyo ni hatari, na kuitaka mahakama kuwapa maafisa wa upelelezi wa ATPU muda zaidi kukamilisha uchunguzi wao.
Hakimu Richard Odenyo alikubali ombi hilo na kuagiza mshukiwa huyo kuzuiliwa kwa siku 30 katika kituo cha polisi cha Kilindini.
Abdalla alitiwa mbaroni na maafisa wa ATPU akiwa na bunduki, risasi, simu, na kemikali zinazoaminika kutengeneza vilipuzi na kipakatalishi, zote zikiaminika kutumika katika kutekeleza ugaidi jijini Mombasa.
Kesi yake itasikilizwa Februari 8, 2016.