Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume anayedaiwa kumlaghai jamaa mmoja zaidi ya Sh100,000 alifikishwa mbele ya mahakama moja ya Nakuru siku ya Ijumaa kujibu shtaka hilo.

Upande wa mashtaka uliarifu mahakama kwamba mshtakiwa, George Maina Kiboche, anadaiwa kumlaghai Samuel Kipng’etich Sh129,785 akidai kwamba angemuuzia gari lenye thamani hiyo, akijua kwamba hakuwa na nia ya kutekeleza hilo.

Kulingana na upande wa mashtaka, mshukiwa huyo alitekeleza kosa hilo kati ya tarehe Septemba 16 na tarehe Octoba 17, 2015 mjini Nakuru.

Kiboche alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu mkuu Alice Towett ambaye alimwachilia kwa bondi ya Sh200,000.

Kesi hiyo itatajwa Novemba 12, 2015 na kuskizwa Januari 21, 2016.