Share news tips with us here at Hivisasa

Mshukiwa wa wizi wa mabavu ameachiliwa huru katika mahakama ya Mombasa baada ya kukinzana kwa ushahidi wa mashahidi wa kesi hiyo.

Akitoa mwelekeo huo, hakimu katika mahakama ya Mombasa Richard Odenyo alisema kuwa ushahidi uliotolewa hauambatani, na unaonyesha wazi kuwa mshukiwa huyo hakuhusika katika uahalifu huo.

Omar Mohammed na wenziwe ambao hawakuwa mahakamani wanadaiwa kuiiba shilingi 6,100, simu na viatu, yote ikiwa ni mali ya thamani ya shilingi 23,000 ambayo ni mali ya Saidi Omar mnano Januari Mosi Mwaka 2013.

Kesi hiyo kwa sasa imetupiliwa mbali na mshukiwa yuko huru.