Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mahakama kuu ya Mombasa imemfunga mshukiwa wa wizi wa pikipiki kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kukiri kutekeleza wizi huo.

Emmanuel Otieno Agumba alidaiwa kuiba pikipiki hiyo yenye thamani ya shilingi 98,000 mnamo Oktoba 5, 2015 katika eneo la ufuo wa bahari wa Shelly huko Likoni.

Emmanuel alikubali makosa hayo siku ya Jumanne mbele ya hakimu Richard Odenyo na kupatilizwa kifungo hicho.

Mshukiwa yuko na siku 14 za kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.