Mwanamume mmoja Jumatano aliponea kuchomwa na wananchi wenye ghadhabu katika mji wa Matuu kaunti ndogo ya Yatta baada kudaiwa kuiba mapipa mawili ya maji katika duka moja.
Inaarifiwa kuwa mwanamume huyo alionekana alipokuwa akitekeleza wizi huo na kuvamiwa.
Akidhibitisha kisa hicho OCPD wa Yatta Edward Changach alisema kuwa maafisa was polisi walikuwa na kibarua kigumu kumwokoa mshukiwa huyo aliyekuwa akipata kichapo kutoka kwa umma.
Aidha Changach aliwaonya washeria mikononi mwao huku akiwaonya walio na tabia ya kupora mali ya wenyewe.
"Mshukiwa alikuwa kamwagiwa mafuta tayari kuchomwa pale polisi walimwokoa,ni vibaya watu kupenda vya bure," Changach alisema.