Share news tips with us here at Hivisasa

Jamaa mwenye umri wa miaka 16 alifikishwa mbele ya mahakama ya Nakuru Ijumaa kwa madai ya kuwabaka watoto wawili.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwabaka wasichana wawili wenye umri wa miaka saba kati ya Februari 1 na 3 katika eneo la Kambi Somali.

Hata hivyo, upande wa mashtaka umetaka mahakama kuagiza mshtakiwa huyo afanyiwe uchunguzi wa kubaini miaka yake halisi kwani kulingana na upande wa mashtaka, jamaa huyo anadai kuwa mwenye umri wa miaka 16.

Mshtakiwa huyo hata hivyo alikana shtaka hilo mbele ya hakimu mkuu wa Nakuru Maroro Nyakundi ambaye aliagiza mshtakiwa afanyiwe uchunguzi wa miaka yake halisi.

Aidha, hakimu huyo mkuu aliagiza mshtakiwa huyo azuiliwe katika rumande ya watoto iliyo kwenye mtaa wa bondeni viungani mwa mji wa Nakuru.