Mshukwa mmoja wa mauaji Mohamed Bakari Bin ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 500,000 katika mahakama kuu ya Mombasa.
Hii ni baada ya wakili wake Pascal Nabwana kuwasilisha ombi la kupewa dhamana mteja wake siku ya Jumanne mbele ya jaji katika mahakama kuu ya Mombasa Dora Chepkwony, kwa kusema kuwa ni haki kwa mteja wake kupewa dhamana kwa mujibu wa katiba.
Mshukiwa huyo anadaiwa kuwa Disemba 4 mwaka jana, alimuua Mahamoud Bakar katika eneo la Mwandoni.
Mohamed alikanusha mashtaka hayo ya mauaji mbele ya jaji Martin Muya siku ya Ijumaa wiki iliyopita.
Kesi yake inatarajiwa kusikizwa tena baadae mwezi huu.