Share news tips with us here at Hivisasa

Huduma ya ukusanyaji wa ushuru kwa njia ya kidijitali ambayo inatumika katika kaunti ya Nakuru imeimarisha ukusanyaji wa ushuru kwenye kaunti hio.

Stephen Maritim ambaye ni waziri wa teknolojia ya mawasiliano katika kaunti ya Nakuru alisema baada ya huduma hiyo kuanzishwa rasmi Januari mwaka jana kwenye kaunti ya Nakuru , ushuru uliongezeka kutoka shilingi bilioni moja nukta nane hadi shilingi bilioni mbili nukta mbili.

Aidha, alikariri kuwa wanatarajia ushuru huo uongezeke mwaka huu huku akiwahimiza wakaazi wa Nakuru kulipa ushuru kupitia kwa mfumo huo ili waweze kupata huduma bora.