Mtoto mvulana wa miaka minne alipatikana akiwa ameaga dunia kwenye mto Esise katika kaunti ndogo ya Borabu, kaunti ya Nyamira mapema Jumamosi wiki jana baada yake kupotea kutoka nyumbani kwao kwa siku moja. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akithibitisha kisa hicho, afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Anthony Onyango alisema huenda mtoto huyo alisombwa na mafuriko ya mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo hilo, huku akiongeza kusema kuwa wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha mtoto huyo. 

"Mtoto mwendazake alipatikana kwenye mto Esise baada yake kutoweka kutoka nyumbani kwao siku ya Ijumaa jioni, na tunashuku kwamba huenda alisombwa na mafuriko ya maji, hali iliyosababisha kifo chake na tayari tumeanzisha uchunguzi kubaini chanzo halisi,"alisema Onyango. 

Onyango aliongeza kusema kuwa marehemu alizikwa kwenye kaburi ya waislamu siku yiyo hiyo kutokana na tamaduni za waislamu. 

"Mwendazake alizikwa kwenye kaburi ya waislamu siku hiyo ya Jumamosi kutokana na tamaduni zao," aliongeza Onyango.