Wakaazi wa eneo la Ituusya katika kaunti ndogo ya Kangundo wameagizwa kuhakikisha wameweka ua katika visima ili kuepuka watoto wachanga kutumbukia ndani.
Haya yalisemwa na chifu wa kata ya Kanzalu Josphine Thomas baada ya mtoto wa umri wa miaka mbili na nusu kufia njiani huku akikimbizwa hospitalini baada ya kuokolewa na wakaazi baada ya kutumbukia kisimani katika eneo hilo.
Chifu huyo alisema kuwa mtoto huyo alimfuata babake alipokuwa akienda kazini mwendo wa asubuhi pale alitumbukia kisimani.
Wakaazi wa eneo hilo walikimbia kumwokoa mtoto huyo aliyeaga dunia kabla ya kufika hospitalini.
Mwili wa mtoto huyo ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Kangundo level four.