Kuna haja ya vipengee vya katiba kuhusu wafanyikazi wa umma na kile cha kupambana na ufisadi nchini kufanyiwa marekebisho ili kuzuia uharibifu wa fedha za umma.
Hii ni kauli ya kinara wa chama cha Amani National Congress Musalia Mudavadi, ambaye ametaja uharibifu wa fedha za umma unaotekelezwa na wabunge katika matumizi yao ya bunge kama njia moja ya kumkandamiza mwananchi.
Akizungumza katika shule ya upili ya Lunguma huko Tsimba, Mudavadi alisema vipengee hivyo ndivyo vinatoa mwanya kwa wafanyikazi wa umma kama vile wabunge kutekeleza ufisadi serikalini.
Kinara huyo aidha alisema kuna haja ya kiongozi kutangaza mali yake kabla ya kuingia afisini kama njia ya kuzuia ufisadi.
Kauli hii inajiri baada ya kushudiwa idadi kubwa ya viongozi serikalini kuhusishwa na ufisadi nchini.