Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Baada ya Rais kuwaahidi makuu viongozi wa kaunti ya Lamu walipokutana katika ikulu ya mombasa mapema wiki hii, viongozi hao wameeleza matumaini yao kuhusiana na ziara yake eneo hilo kuwa itatatua tatizo la uskwota na ukosefu wa usalama.

Naibu gavana wa Lamu Eric Mugo pamoja na viongozi wakuu kauntini humo wamesema swala la uskwota litasuluhishwa tu kupitia ugavi wa ardhi na kutoa hati miliki kwa maskwota.

Viongozi hao wamelalama kuwa inavunja moyo kuona ardhi nyingi zinanyakuliwa na mabwenyenye hivyo kuwaacha wakazi wazaliwa wa kaunti hiyo kuwa maskwota katika ardhi zao wenyewe.

Rais anatarajiwa kuzuru eneo la Lamu hapo kesho alhamisi na Ijumaa ili kutoa hati miliki za ardhi.