Mbunge wa Kilifi Kaskazini Gideon Mung’aro amesema atahakikisha uchaguzi mkuu ujao chama cha JAP kitashinda eneo zima la Pwani.
Hii ni kuondoa fikra za baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaodai kuwa eneo hilo ni ngome ya ODM.
Akizungumza na wanahabari siku ya Jumanne, Mung'aro ambaye pia ni mwenyekiti wa wabunge wa Pwani alisema kuwa japo JAP alishindwa katika uchaguzi mdogo wa Malindi uliyofanyika siku ya Jumatatu bado wakaazi wa Pwani wanaimani na JAP kuwa chama chao na lazima uchaguzi mkuu ujao kunyakua ushindi huo.
Mung'aro alisistiza kuwa ukanda wa pwani umejitolea kakamilifu kujiunga na chama kipya cha JAP katika uchaguzi mkuu ujao hivyo basi chama cha ODM pia kikubali kushindwa katika uchaguzi mkuu ujao kama vile chama cha JAP kulivyokubali kushindwa katika uchaguzi mkuu ujao kwani viongozi wa chama hicho wanajiandaa kubadili fikra za watu kuwa eneo la Pwani ni ODM.
"Wakazi wa pwani wametuambia kuwa wanaunga mkono chama kipya cha JAP sasa lengo letu ni kuhakikisha kuwa Pwani kwa jumla katika uchaguzi ujao unakuwa ndani ya serikali kwa kukipigia maswala muhimu ya wapani kupitia chama cha JAP,’’ alisema Mung’aro.
Aidha, aliwahakikishia wakaazi kuwa ahadi zote walizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Malindi zitatimizwa na uchaguzi mkuu chama cha JAP kuinachukua uongozi pwani.
Wakati huo huo alitanga kuwania kiti cha ugavana wa kaunti ya Kilifi na akawarai wakaazi wa kaunti ya Kilifi na eneo zima la pwani kumuunga mkono na kumchagua katika uchaguzi mkuu ujao ili kuwafanyia wakaazi maendeleo.
"Ninawaomba wakaazi wa kaunti ya Kilifi na eneo zima la pwani kunichagua kama gavana wa kaunti ya kilifi katika uchaguzi mkuu ujao ili tufanye kazi kwa pamoja na kuwaondoa wale viongozi wabinafsi," iliongeza Mung'aro.