Wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka eneo bunge la Borabu wameweka mipango ya kutembelea shule mbalimbali katika eneo hilo ili kuwapa wanafunzi ushauri.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubu siku ya Jumatano, mwenyekiti wa muda wa muungano huo Emily Nyaboke, alisema kuwa watafanya utafiti ili kubaini chanzo cha matokeo ya mitihani yasiyo ya kuridhisha.

"Tumeamua kutembele shule zote kuwapa wanafunzi ushauri na kuwahimiza kutia bidii kwenye masomo yao. Tuna furaha kwamba mbunge wa eneo hili ameahidi kutuunga mkono na kwa kweli tutatumia fursa hiyo kufanya utafiti kuhusiana na ni kipi kinachofanya wanafunzi kutopasi mitihani ya kitaifa," Alisema Nyaboke.

Nyaboke aidha aliwasihi washikadau kujitokeza na kuuunga mkono muungano huo wa vijana, ili iwe rahisi kutekeleza wajibu wao.

Aidha, alisema kuwa watafanya juhudi za kuwapokeza walimu bidhaa zitakazo warahisishia kazi zao.

"Mpango huu wa kuzitembelea shule sio tu wakuwapa ushauri wanafunzi bali pia wa kuwapokeza walimu na wanafunzi vitabu na karatasi za mitihani, zitakazo wasaidia kufanya marudio kabla ya wanafunzi kufanya mitihani ya kitaifa. Tunaelewa kuwa shule nyingi zina upungufu wa vitabu na karatasi za marejeleo," alisema Nyaboke.