Muungano wa kitaifa wa wafanyibiashara umempongeza waziri wa utalii Najib Balala kwa kuanza kurudisha hadhi ya Mombasa kwenye kiwango chake cha hapo awali.
Kwenye kikao na wanahabari afisini mwake siku ya Jumatatu, mwenyekiti wa muungano huo James Mureu alisema kuwa mwishoni mwa mwaka uliopita, Mombasa iliweza kupokea meli tatu ambazo waziri Balala alizikaribisha, kuonyesha kuwa yuko tayari kwa kazi hiyo.
Aidha wamempongeza Rais kwa kuendeleza kuweka mataa kote katika eneo hilo,jambo ambalo pia linakuza biashara kwa masaa 24, na kumtaka sasa kuhakikisha usalama umedumishwa nyakati za usiku,
Wakati huo huo, amewataka wanasiasa kuepuka malumbano ya kisiasa kwa sasa na kuwafanyia watu maendeleo, na kuwapa nafasi za kufanya biashara huku wakisubiri mwaka 2017 ambapo kutakuwa na uchaguzi.