Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 15 alijitia kitanzi siku ya Jumatatu katika eneo la Manga kaunti ya Nyamira baada ya kudaiwa kutishiwa maisha na jirani yake.
Akitibithisha kisa hicho siku ya Jumatatu chifu wa lokesheni ya Kitutu Evans Nyanga’u alisema mtoto huyo ambaye alikuwa anasoma shule ya msingi ya Bigogo wilayani Manga akiwa darasa la nane alitishiwa maisha na jirani yake baada ya kufuta nyimbo kwenye simu.
Mtoto huyo alimfahamisha baba yake dhidi ya kutishiwa maisha na jirani yake.
“Ripoti ambazo tuko nazo ni kuwa mtoto huyu aliamua kujitoa uhai baada ya jirani yake kumtishia maisha yake baada ya kufuta nyimbo ambazo zilikuwa kwa simu yake na kumtishia maisha yake ,”alisema chifu Evans Nyang’au.
Aidha, chifu huyo alisema jirani huyo aliposikia kisa hicho kimetendeka alitoroka huku juhudi za kumsaka zikishika kasi.
Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Nyamira level five huku uchunguzi ukiendelea kuhusiana na kisa hicho ya kutatanisha katika eneo hilo.