Kijana wa miaka kumi na saba aliaga dunia katika bwawa la Katindi Moja katika ene la Katindi, kata ya Kiima kimwe pale alipokuwa akiogelea.
Akidhibitisha kisa hiki baada ya kufika pale, chifu wa Kata ndogo ya ya Mbilini Antony Muasa alisema kuwa mvulana huyo alikuwa ametumwa sokoni na mamake mwendo wa saa kumi na mbili jioni huku akiwa na rafiki zake.
Chifu Huyo alielezea kuwa mvulana huyo aliamua kuogelea japokuwa rafiki zake walijaribu kumsihi asiogelee kwani giza lilikuwa linabisha hodi.
Kijana huyo alipozama hakuibuka pale marafikize walishikwa na hofu na kupiga ukemi kuitisha msaada, ndiposa wakazi waliwasili lakini kijana alikua kakata kamba.
"Mvulana huyo alikuwa tayari mfu alipookolewa na watu waliofika baada ya kuskia nduru," alisema Muasa.
Muasa alisema kuwa viongozi hawafai kungoja hadi pale majanga yametendeka ili kuchukua hatua, kwani wakazi wa eneo hilo kwa mda mrefu wamekua wakiagiza bwawa hilo kuekewa ua ili kuzuuia maafa.
Mwili wa mvulana huyo ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Machakos level five.