Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwakilishi wa wadi ya Sensi Kaunti ya Kisii Nyagaka Onchong’a amewashauri vijana katika wadi yake kuunda vikundi kadhaa vya vijana ili kuweza kufaidika na fedha za serikali za miradi kwa vijana za Uwezo ili kujiendeleza na kujiimarisha kimaisha.

Sasa vijana hao, ambao wamekua wakilaumu serikali ya Kaunti ya Kisii kwa 'kuwaacha nje' wakati wa usambazaji wa fedha za maendeleo ya vijana almaarufu Uwezo Fund wametakiwa kuanzisha na kujiunga na vikundi vingine vilivyoundwa tayari ili kufaidika na pesa za miradi kwa vijana ili kujiendeleza kimaendeleo na kimaisha.

Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumanne mjini Kisii, Ochong’a alisema ikiwa vijana wanahitaji kumaliza umaskini sharti wajiunge kwa vikundi ili kupata pesa za serikali kufanyia biashara

“Naomba vijana katika wadi yangu waweze kujiunga kwa vikundi ili wapate pesa kutoka kwa serikali na kuanza biashara au kilimo chochote na kujiendeleza kimaisha,” alisema Ochong'a.

Mwakilishi huyo alisema hakuna haja kwa vijana kusema wanaishi katika hali ya umaskini kwani ni wao hawajawajibika kwa kujitolea kujiendeleza na biashara.

Onchong’a aliomba afisi za Kaunti ya Kisii, haswa zile zinazosimamia hazina hiyo kurahisisha kazi kwa kuwajibikia vikamilifu sheria zilizowekwa wakati wananchi wanapohitaji kutumikiwa ili yeyote asiachwe nyuma na maendeleo ya serikali kwa umma na kupunguza umaskini miongoni mwa wanachi wote nchini.