Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwakilishi wa Wadi ya Sensi Onchong’a Nyagaka amewakosoa baadhi ya wanasiasa ambao wanamlaumu kufuatia shule za wadi yake kutofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa.

Akizungumza siku ya Jumanne, Nyagaka aliwaonya wanasiasa hao dhidi ya kumuhusisha na masuala ambayo hayafahamu, na kusema kuwa sekta ya elimu husimamiwa na serikali ya kitaifa.

“Sekta ya elimu husimamiwa na serikali ya kitaifa. Wale ambao wananilaumu kwa vile shule za wadi yangu hazijafanyi vyema katika mitihani ya kitaifa wakome kwani kazi yangu ni kuhakikisha nimefanya maendeleo kwa kuwakabidhi wanafunzi fedha a za basari ili waendeleze masomo yao,” alisema Nyagaka.

Nyagaka aliomba wazazi kushirikiana na walimu ili kuinua viwango vya elimu katika shule za wadi hiyo, na kuwataka kutosikiza wanasiasa wanao endeleza siasa zisizo sheheni maendeleo.