Swala la elimu kwa mtoto wa kike lafaa kupigwa jeki katika wadi zote za kaunti ya Nakuru.
Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wadi ya Elburgon Florence Wambui, ambaye anasema kuwa mtoto wa kike hupitia changamoto nyingi hasa mashinani.
Anaongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba baadhi ya watoto wa like hukosa kuenda shule kuwa kukosa vitambaa vya hedhi ama sodo.
Amesema kuwa kila wadi inafaa kutenga fedha za kushughulikia swala hilo ili kuhakikisha kila mtoto wa kike anapata elimu.
"Ninajua mtoto wa like anapitia msaibu si haba katika kupata elimu, ndiposa nawarai viongozi wenzangu tushirikiane katika kuhakikisha watoto wetu hawapitii changamoto epuka.
Alikuwa akizungumza katika mkutano wa kijamii huko Elburgon, na alitoa wito kwa kila mmoja katika jamii kujali maslahi ya watoto.