Mwakilishi wa walemavu katika bunge la Kaunti ya Nakuru Emmah Mbugua ametaka sheria na sera za walemavu kushughulikiwa haraka ili kuwafaidi wanaoishi na changamoto ya ulemavu.
Akizungumza Jumamosi wakati wa kuwakabidhi walemavu vifaa mbalimbali vya kuwasaidia kutembea, Mbugua, ambaye pia anaishi na changamoto ya ulemavu wa macho, alisema kuwa kutopasishwa kwa sheria hizo ni pigo kwao.
"Ningependa kuwaomba wanachama wenzangu wa bunge la Kaunti ya Nakuru kwamba tushughulikie sheria za walemavu," alisema Mbugua.
Wakati huo huo, Mbuguah alipongeza familia ya Bwana na Bi David Talbot kutoka marekani ambao walitoa vifaa vya walemavu kwa jamii ya walemavu katika kaunti hiyo.
Vifaa hivyo vitasambazwa katika kila kaunti ndogo zote kuwafaidi walemavu.