Mwalimu mmoja wa shule ya msingi ya Kinyui mwenye umri wa miaka hamsini alitiwa mbaroni na maafisa wa polisi hapo siku ya alhamisi alipopatikana amelewa masaa yasiofaa katika eneo la Kinyui kaunti ndogo ya Matungulu.
Akidhibitisha kisa hiki chifu wa kata ya Tala Pius Nzioka alisema kuwa mwalimu huyo anayetambulika kama Bernard kivuva alisubiri wakati walimu walikuwa na mkutano wa elimu pamoja na wazazi mchana pale alitumia nafasi hiyo kutoroka na kwenda kulewa kabla ya kutiwa mbaroni.
Aidha, Nzioka alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona walimu wanaotarajiwa kuwa mfano mwema kwa wanafunzi kutenda jambo la aibu kama hili.
"Mwalimu anapofanya kitendo hiki anajikosea heshima hasa kutoka kwa wanafunzi wanaomtazamia," alisema Nzioka.
Chifu huyo alitaka walimu kuwa mfano wa kutajika kwa wanafunzi ili waweze kuheshimiwa na kujiepusha na mambo yasiyofaa kama kuja darasani wakiwa walevi na mengineo.
Kwa sasa mwalimu huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kangundo akisubiri kufikishwa kortini.