Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Moi Stephen Karanja amekosoa vyombo vya habari kwa kudai kwamba ameongeza karo. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza siku ya Ijumaa wakati wa kikao na wanafunzi wa kidato cha nne na tatu, Karanja alitaja swala hilo kama uvumi usio na misingi wowoote. 

"Hata watu wa vyombo vya habari wameandika eti Karanja ameongeza karo, najua ni propaganda tu maanake hawana ukweli kwa madai hayo," alisema Karanja. 

Aidha aliongeza kuwa karo ya shule hiyo ni kwa mujibu wa chapisho rasmi la serikali wala hajaongeza chochote, na kuwataka wanahabari kuwajibika na kupata maelezo kamili wanaporipoti. 

"Marafiki wangu wa vyombo vya habari nawaheshimu lakini mnafaa kupata maelezo kikamilifu," aliongeza Karanja. 

Wakati huo huo, amewataka wazazi kuzuru shuleni kila mara ili kujua baadhi ya maendeleo yanayopewa kipau mbele.

Itakumbukwa ni hivi maajuzi ambapo wazazi walilalama kuhusu viwango vya juu vya karo na kupelekea wizara ya elimu kuingilia kati.