Kiti cha eneo wakilishi wadi Solai kaunti ya Nakuru kimeanza kuwavutia wagombea kadhaa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanahabari na mwanablogi Kelvin Waweru maarufu Kel Wesh alisema kuwa atawania kuwa MCA wa eneo hilo.

Akihutubia wanahabari katika kijiji cha lower Solai,Waweru anasema kuwa lengo kuu la kuwania kiti hicho ni kuleta maendeleo maeneo hayo. 

Amemshtumu mwakilishi wa wadi hiyo wa sasa kwa madai kwamba anaendeleza ukabila na siasa potovu.

 "Mimi nashangaa sana mtu akijiita kiongozi wa Solai na ilhali hata hakuna maendeleo hapa," Waweru alisema.

 Wakati huo huo ameunga mkono shinikizo za kutaka vikosi vya usalama KDF vilivyo somalia kurejea humu nchini. 

Kwa mujibu wake, serikali imetumia fedha nyingi kugharimia vikosi hivyo na wakati ni sasa kwa njia mbadala ya kutatua swala la ugaidi humu nchini.