Mwanaharakati wa haki za binadamu Masese Kemunche ametoa wito kwa jamii kuwajibika na kuhakikisha viongozi wanatekeleza wajibu wao.
Akizungumza Jumatano wakati wa hafla ya kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wao katika uongozi, Masese amesema kuwa wakati viongozi wanakosa kuwajibika,wa kulaumiwa ni mwananchi kwa kukosa kuwawajibisha.
"Mara nyingi sisi husema viongozi wamefeli, lakini ukweli wa mambo ni kwamba si wao bali ni sisi wananchi," Masese alisema. Mwanaharakati huyo ambaye pia ni mpanga ratiba katika shirika la Centre for Enhancing Democracy and Good Governance-CEDGG alisema kuwa ni jambo la busara kwa viongozi pia kutoa mwongozo au mwelekeo mwema kwa wananchi.