Hatimaye mwanajeshi mmoja wa kikosi cha KDF kutoka eneo la Likoni aliyeuwawa katika shambulizi la wiki jana El Adde amezikwa nyumbani mwao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Marhuma Juma Bakari alifikishwa nyumbani kwake eneo la Kona Mpya wilayani humo mnamo adhuhuri ya Alhamisi tayari kwa sherehe za mwisho.

Biwi la simanzi lilitanda kote huku watu wakimmiminia sifa tele shujaa mwendazake.

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho na mwakilishi wa akina mama Mishi Mboko walikua miongoni mwa waombolezaji waliojumuika kuifariji familia.

Aliyeongea kwa niaba ya familia aliishukuru serikali kuu na ile ya kaunti ya Mombasa kwa kuharakisha shughuli ya uchunguzi wa miili na kuwawezesha kumtambua mpendwa wao.