Mwanamke mwenye umri wa takriban miaka 45 amehukumiwa kifungo cha miaka kumi gerezani na Mahakama ya Mombasa.
Mshtakiwa huyo, Regina Muthengi, alipatikana na kosa la kumyanyasa kimapenzi mwanafunzi wa miaka mitano.
Muthengi ambaye ni mhudumu wa watoto katika shule ya kibinafsi ya Shelly Beach Academy iliyoko Likoni, anadaiwa kupapasa sehemu za siri za mwanafunzi huyo kati ya Machi 18 na 21 mwaka 2011.
Akitoa hukumu hiyo siku ya Ijumaa, hakimu mkuu wa mahakama ya Mombasa Susan Shitub, alisema kuwa ushahidi uliotolewa unaonyesha kuwa mshukiwa alihusika katika kitendo hicho.
Mshukiwa huyo alipewa siku 14 za kukata rufaa kupinga kifungo hicho.