Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamke mmoja amefikishwa mahakamani kwa shataka la kujaribu kumua mumewe.

Upande wa mashtaka ulieleza mahakama kuwa kati ya Oktoba 20, 2015 na Oktoba 26, 2015, mshukiwa, Rose Adhiambo, ambaye ni mke wa Polycarp Okumu, akiwa ameshirikiana na mfanyikazi wake wa nyumbani, Doris Akinyi, wanadaiwa kupanga njama na majambazi ili kumvamia Okumu katika eneo la Nyali.

Wawili hao walikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkuu wa Mombasa Susan Shitub siku ya Jumatau.

“Hatukuhusika kamwe na njama hiyo,” walisema washtakiwa.

Washukiwa hao watasalia rumande hadi Novemba 11, 2015 kusubiri uamuzi wa kupewa dhamana.