Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamke wa umri wa makamo amefunguliwa mashtaka ya mauaji katika Mahakama kuu ya Mombasa.

Mshtakiwa, Teresia Mukulu, anaidaiwa kumuua Benard Nyongesa mnamo Novemba 6, 2016, katika eneo la Mwamambi, huko Diani, Kaunti ya Kwale.

Mshtakiwa huyo alikanusha madai hayo siku ya Alhamisi mbele ya Jaji Martin Muya.

Kesi yake itasikizwa tarehe Juni 29, 2016.