Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamke mwenye umri wa miaka 27 amehukumiwa miaka 7 gerezani kwa kosa la mauaji ya mumewe.

Mshukiwa, Agness Mutheu, anadaiwa kumdunga kisu hadi kufariki mumewe Antony Hanjari, mnamo Machi 16, 2013 katika eneo la Kisauni.

Akitoa hukumu hiyo siku ya Jumatatu, jaji Martin Muya alisema kuwa kulingana na ushahidi uliotolewa, ni wazi kuwa mshukiwa alihusika katika mauaji hayo wakati alipokuwa amelewa.

Aidha, alimpa mshtakiwa siku 14 za kukata rufaa kupinga kifungo hicho.

Mshatakiwa Agnes Mutheu, alishikilia msimamo wake wa kutohusika katika mauaji hayo ya mumewe, na kuiambia mahakama kuwa walikuwa wanapendana na mwendazake.