Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamke mwenye umri wa miaka ishirini na tano hii leo amefikishwa mbele ya mahakama kuu ya Kisumu kujibu mashataka ya kuchapa na kuwajeruhi wanawe wawili.

Maryanne Akinyi mkaazi wa Manyatta Kisumu alikanusha mashataka hayo mbele ya hakimu mkuu wa Kisumu Thomas Obutu.

Mshatakiwa anadaiwa kutekelekeza makosa hayo kati ya Tarehe ishirini Desemba mwaka jana na tarehe kumi na nne Februari mwaka huu.

Kulingana na upande wa mashataka, Akinyi amekuwa akiwachapa wanawe kwa muda huo huku akiwajeruhi, kisa kilichopelekea watoto hao kulazwa hospitalini.

Watoto hao wa kiume wenye umri wa miaka sita na tano, waliokolewa na majirani walio ripoti kisa hicho kwa polisi.

Sasa hivi watoto hao wako chini ya ulinzi wa idara ya watoto Kisumu.

Upande wa mashtaka uliitaka mahakama kumuzulia mshatakiwa kwa muda wa wiki mbili ili kuezesha ukamilifu wa uchunguzi.

Akipinga Ombi hilo, Akinyi aliiambia mahakama kuwa alikua anawalea wanake kwa njia iliyo sawa kwa kuwapatia adabu maanake aliwachapa kidogo.

Akinyi alisema kuwa majeraha wanawe waliyapata kutokana na kucheza ila si na kuchapwa. 

Alisema kuwa majirani walioripoti kisa hicho wana wivu maanake ako na watoto wazuri.

Obutu alimuzuilia korokoroni kwa muda wa wika moja, atakapo rejea mahakamani ombi lake la kuachiliwa kwa dhamana litasikizwa.

Kesi hiyo itarejelewa wiki ijayo Alhamisi.