Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamke wa umri wa makamo amepatikana na makosa ya mauwaji ya mmewe katika mahakama ya Mombasa.

Mnamo Machi 16, 2013 katika eneo la Kisauni, Agness Mutheu anadaiwa kumdunga kisu hadi kufariki mmewe Antony Hanjari.

Akitoa uamuzi huo siku ya Alhamisi, jaji katika mahakama kuu ya Mombasa Martin Muya alisema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa unaonyesha kuwa mshukiwa alihusika katika mauwaji hayo bila kukusudia.

Agnes alishikilia msimamo wake wa kutohusika katika mauwaji hayo ya mmewe, na kuiambia mahakama kuwa walikuwa wanapendana na marehemu mwendazake.

Mahakama kuu inatarajiwa kutoa hukumu yake Februari 8, 2016.

Kwa sasa Agnes atazidi kuzuiliwa katika gereza la Shimo La Tewa.