Mwanamume mmoja amefikishwa katika mahakama ya Mombasa kwa madai ya kuhusika na wizi.
Januari 9, 2016 katika eneo la mzunguko wa Docks Kilindini, Japheth Kithi Kitsao pamoja na wenzake ambao hawakuwa mahakamani wanadaiwa kuiba njugu zenye thamani ya shilingi 70,000 kutoka kwa gari aina ya lori.
Inadaiwa kuwa mali hiyo ilikuwa ni ya Tarus Kipchirchir ambayo ilikuwa ikisafirishwa kutoka afisi ya shirika la chakula ulimwenguni WFP zilizoko mjini Mombasa ambayo ilikuwa ikisafirishwa katika kambi ya wakimbizi iliyoko nchini Somalia.
Mtuhumiwa alikana madai hayo mbele ya hakimu Richard Odenyo, katika mahakama ya Mombasa na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 100,000.
Kesi hiyo itasikilizwa Januari 28,2016.