Mwanamume mmoja alifikishwa mahakani Mombasa siku ya Jumanne kwa tuhuma za kupatikana na ngozi ya chui.
Upande wa mashtaka uliiambia mahakama kuwa mnamo Disemba 28, 2015, mshukiwa huyo, Samson Juma Baya alipatikana na ngozi ya chui yenye thamani ya shilingi 100,000 katika eneo la Kizingo, jijini Mombasa.
Baya alikanusha madai hayo mbele ya hakimu Samuel Rotich na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 1,000,000.
Mshukiwa huyo alitiwa mbaroni siku ya Jumatatu eneo la Kizingo jijini Mombasa.
Kesi hiyo itasikilizwa mnamo februari 10,2016.