Mwanamume mwenye umri wa makamo amefungwa kifungo cha maisha baada ya kupatikana na makosa ya mauwaji.
Mnamo Oktoba 22 mwaka 2012, Julius Shukran Mganga anadaiwa kumuuwa Osman Salat Hanish katika mtaa wa Mbaya Mose huko mjini kilifi.
Akitoa hukumu hiyo siku ya Jumatatu, jaji Martin Muya alisema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa unaonyesha kuwa mshukiwa alihusika katika mauwaji hayo.
Jaji Muya alimpa mshukiwa siku 14 za kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.