Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamme wa umri wa makamu ameokolewa na wapiga mbizi katika kivuko cha feri cha Likoni baada ya kujaribu kijitoa uhai kwa kujitupa ndani ya bahari kutoka kwa feri ya Mv Nyayo aliyokuwa ameabiri.

Kulingana na waliyoshuhudia kisa hicho walisema kuwa mwanamume huyo aliabiri feri hiyo, kisha akaonekana kusonga katika eneo lisiloruhiswa abiria kuteti kabla ya kijitupa ndani ya bahari.

"Sisi tumeona mtu akisongea karibu na mahali ambapo watu walikatazwa kuteti kisha baadaye naskia kama kitu kimeingia ndani ya bahari kusonga kuangalia ndio nikaona wapiga mbizi wakijitosa ndani ya maji kisha wakatoka na huyo mwanaume, hata sijui kama alikuwa na matatizo gani," alieza Mariam Khamis, mmoja wa abiria.

Mwanamume huyo alipelekwa kwa kituo cha polisi cha feri kueleza bayana sababu za kutaka kujitoa uhai katika kivuko hicho kabla ya kupelekwa hospitali kupima akili kwani inadaiwa kuwa huenda alikuwa na akili punguani.

Maafisa wa polisi wamewaonya wakazi wanaovuka katika kivuko hicho kuwa waangalifu na iwapo wanashida flani basi wawasiliane na maafisa wanaoshika doria katika kivuko hicho ili kuzuia kushuhudiwa majanga.