Share news tips with us here at Hivisasa

Polisi mjini Molo wanamzuilia mwanamume mwenye umri wa makamo kwa tuhuma za kumbaka mjakazi wake mwenye chini ya umri alipokuwa amelala kwenye chumba chake mwendo wa saa kumi na moja asubuhi.

Mwadhiriwa ameeleza jinsi mwajiri wake alivyoingia kwenye chumba chake cha kulala na kumwamsha huku akiwa uchi wa mnyama.

“Nikiwa na maruerue ya usingizi nilipatwa na mshangao mkubwa nilipompata mzee wa nyumba akiwa kando ya kitanda changu baada ya mkewe kurauka mapema na kuelekea kazini,” msichana huyo alisema.

Habari zaidi zinasema jamaa huyo alijitoza kitandani na kumfunga mdomoni msichana huyo mwenye umri wa miaka 16 kabla ya kumdhulumu kimapenzi.

Mwathiriwa alisema baada ya kufanyiwa unyama huo alielekea kwa jirani mmoja ambaye alisikitishwa na tukio hilo huku akiulizwa kuelekea na kutoa riporti kwenye kituo cha polisi cha Molo kabla ya kupata matibabu.

Mjombake msichana huyo ameitaka idara ya polisi kufanya uchuguzi wa kina na kumchukulia mshukiwa hatua kali za kisheria.

Amesema mshukiwa alikabiliwa na kosa lingine la ubakaji miaka miwili iliyopita, na licha ya kufikishwa katika kituo cha polisi, hakufikishwa mahakamani ili hatua ichukuliwe dhidi yake.

Diwani wa zamani wa wadi ya Molo Charles Njenga amekashifu ongezeko la visa vya ubakaji mjini Molo huku akiitaka idara ya mahakama kuwapa adhabu kali washukiwa wa ubakaji kama hatua moja ya kupunguza visa kama hivyo.

“Mwaka jana zaidi ya wasichana watano wa shule za msingi walibakwa na wakauawa na watu wasiojulikana katika eneo hili letu na inatutia hofu sana,” diwani huyo alisema.

OCPD wa Molo Job Lesikinwa amedhibitisha kutio hilo huku akisema baada ya mshukiwa kukamatwa na wahusika kuandikisha taarifa uchuguzi unaendelea na kwamba mshukiwa atafikishwa mahakamani baada ya uchuguzi kutamatishwa.