Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 46 siku ya Jumatatu aliponea chupuchupu kuuawa na wakaazi baada ya kutuhumiwa kumnajisi mtoto mmoja katika eneo la Kalyambeu, kata ya Ikombe kaunti ndogo ya Yatta.
Akidhibitisha kisa hiki, chifu wa kata hio Onesmus Nzile alielezea kuwa mwanamume huyo anadaiwa kumngojea msichana huyu mwenye umri wa miaka mitatu pale alipokuwa akirejea kutoka shuleni ambappo alimhadaa na kumvuta katika kichaka kimoja kisha kutekeleza unyama huo.
"Alimsubiri mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa chekechea akirejea toka shuleni pale alimhadaa na kumwingiza kichakani ili kumnajisi lakini akafumaniwa," alisema Nzile.
Nzile aidha alisema kuwa kwa bahati nzuri mshukiwa huyo alifumaniwa na wakaazi akiendeleza uovu wake pale walimpa kichapo cha mbwa koko kabla ya kuokolewa na chifu.
Msichana huyo anatibiwa katika hospitali ya Matuu level four huku mshukiwa huyo anayetarajiwa kufika kortini apo kesho akiendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Matuu.