Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamume mmoja atasalia rumande kwa siku 14 baada ya kukamatwa kwa madai ya kumua mchumba wake.

Hii ni baada ya afisa wa upelelezi Martin Ojwang kuomba mahakama impe muda ziadi ili kukamilisha uchunguzi dhidi ya mshukiwa huyo.

Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatano, Hakimu Diana Mochache alimtaka afisa huyo kuharakisha uchunguzi huo ili mshtakiwa kufunguliwa mashtaka ya mauwaji iwapo uchunguzi utabainisha alihusika katika mauaji hayo.

Mahakama ilielezwa kuwa Novemba 8, 2015, katika eneo la Mtongwe huko Likoni, mshukiwa Dancan Matheka anadaiwa kumpiga na kumjeruhi marehemu Christine Mwende mwenye umri wa miaka 29.

Mwende aliaga dunia katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Pwani wakati alopikuwa akipokea matibabu.

Kesi hiyo itatajwa Novemba 25, 2015 ambapo mshukiwa atafunguliwa mashtaka iwapo uchunguzi utabainisha alihusika katika mauaji hayo.